WAZIRI WA UGATUZI ASEMA CHAKULA KIPO KUKABILI NJAA

Serikali jana ilisema kuwa itahakisha kwamba suala la bad la njaa linakabiliwa vilivyo nchini .Akiongea wakati alipozindua mpango wa kugawa chakula kwa wakazi wa Tana River , waziri wa ugatuzi Bw Eugene Wamalwa alisema kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kwamba athari za ukame zinakabiliwa.
"Hatuwezi kuketi chini tukiona wazi kabisa wananchi wanapitia shida. Ndio maana tumeamua kwamba tutatumia kila mbinu kuhakikisha kwamba kuna chakula cha kutosha kusambaza kwa wale ambao wanapitia changamoto kwa sasa," akasema Bw Wamalwa.

Comments