Harakati za baraza la jiji la Mombasa kulisafisha jiji.

Nimevutiwa mno na juhudi zilizoanzishwa na diwani wa wodi ya Kingorani hapa jijini ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mazingira Bw.Said Mathias ambaye ameamua liwe liwalo jiji hili litakuwa safi.

Kwa hakika juhudi hizi zimekuwa zikivutia mno binafsi hasa baada ya miaka mingi ya uvunjaji wa sheria za usafi ambazo zilikuwa zimeleta doa katika juhudi za baraza la jiji hili kuendesha usafi.Kulingana na diwani Mathias,sasa ni marufuku kuvuta sigara ovyo mbali na kumwaga taka katika maeneo ambayo hayajaruhusiwa na baraza.

Juhudi hizi zinafaa kuigwa na kupongezwa na kila mkaazi wa jiji hili la Mombasa.

Comments