JIJI LA MOMBASA SASA LINAMETAMETA

Kwa hakika sasa kila yule anayeingia jijini Mombasa atakubaliana nami kuwa jiji hili sasa linametameta baada ya miundo mbinu ambayo ilikuwa ikitishia jiji hili kuimairshwa maradufu.Baadhi ya mambo ambayo yalikuwa kilio cha wakazi wengi jijini hapa sasa kimesikika.Kwa mfano mataa katika daraja la Nyali hadi katikati mwa jiji sasa yanawaka usiku wote.Hali hii imewaepushia wale ambao walizoea kupigwa tero na vibaki na mikora katika daraja hili la Nyali.Kama daraja ambalo linaunganisha jiji la Mombasa na mitaa ya kasikazini kama Bamburi,Kongowea,Mishomoroni na Kisauni,huwa na wakazi wengi hadi usiku.Na kwa sababu hakukuwa na mataa,wezi walitumia udhaifu huo kuwanyanyasa kabisa wapita njia.Angalau sasa baraza la jiji limefanya kazi nzuri.Nasema ahsanteeni tena sana.

Comments