Tamko la wapwani kutosoma lachemsha watu wa pwani:

Tamko la katibu katika wizara ya ardhi Kombo Mwero kuwa watu wa pwani hawawezi kupata nyadhifa kuu katika afisi za serikali kwa vile hawana elimu limewakasirisha mno wasomi wa mkoa huu ambao sasa wanamtaka katibu huyo aombe msamaha.Katibu Mwero akiongoea katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa pwani wakati wa kongamano la ustawi kufikia mwaka wa 2030,alidai wakazi wa mkoa wa pwani hawajaweza kuajiriwa kazi kubwa kwa kukosa elimu.

Hata hivyo Sheikh mmoja ambaye alisomea sana mambo ya baharini aliinuka na kumkashifu katibu huyo kwa ujeuri huo huku akisema kuwa licha ya yeye kusoma sana,bado hajapata kazi katika shirika kubwa kama vile KPA.

Sasa maoni kwenu watu wa pwani,je? katibu huyu alikuwa na maana gani aliposema watu wa pwani hawakusoma.

Tafadhali leteni mchango wenu katika blog hii ili tuendeleleze hoja hii.

Kazungu Samuel

Comments

Hata Tanzania wanasema watu wa pwani hawajasoma. Ni usemi tu maana siku hizi wengi wamesoma.
Kazungu Samuel said…
Da Chemi,mimi nilidhani ni Kenya peke yake ndiko ambako watu wa pwani wanadharauliwa kuwa hawakusoma kumbe hata pwani ya Tanzania pia ni hivyo hivyo.Haya kwa kweli ni mambo ya kuvunja moyo kwani sasa wapwani hapa wamesoma wengi wakiwa na madigrii lakini ndio hivyo mambo ya kupiga lami kila siku bila ajira.Na hali hii sasa imechangiwa na ukweli kuwa sasa tunakaribia uchanguzi mkuu.shtuma zinatoka kama cheche kutoka kwa wasomi wa pwani ambao wanadai katibu huyu alitumwa kutukana wapwani.