Mambo haya yanafanyika hapa pwani-Kenya.

DONDOO

MARIAKANI-KALOLENI

Hali ya taharuki na wasiwasi ilitanda majuzi katika kituo hiki cha biashara baada ya kiwete mmoja kufika hapo na kamba shingoni akitaka kujinyonga kwa dai la kusalitiwa na mpenzi wake aliyempenda.

Kwa takribani dakika kumi hivi,manamba na watu wa kujitolea walikuwa na wakati mgumu kumtuliza kiwete huyo ambaye alikuwa akilia kwa sauti huku akimuonyesha kila mtu ujumbe ambao alidai aliletewa na msichana ambaye alikwua akipanga kumuoa hivi karibuni.”Kwa kweli kwa jinsi mambo yalivyo sasa,inaonekana mrembo wangu ataniacha tafadhali nisaidieni jamani,” akalia kabla ya kutisha kujitoa uhai.

Miongoni mwa wale waliojipata katikati ya kasheshe hii ya kiwete hii ni jinsi alivyokuwa akionyesha ujumbe huu.Katika ujumbe huu ambao mdokezi wetu aliwahi kuusoma,demu alisema kuwa amekatisha uhusiano na kijana huyo mlemavu bila kuongeza zaidi.”Uhusiano wetu umeisha kwa hivyo sina mengi zaidi ya hayo,tayari nimwaeleza wazazi wangu kuhusu uamuzi huu.” Ikasema sehemu ya ujumbe huu.

Hata hivyo mdokezi wetu aliyekuwa katika shughuli za kikazi mjini Mariakani alilazimia kuondoka eneo hilo kutafuta usafiri kurudi jijini Mombasa,huku akimwacha kiwete huyo akiendelea kupatiwa mawaidha kuhusu hali ya kimaisha na jinsi ya kuepuka dhana hiyo.

Mwisho.

DONDOO

JILORE-MALINDI.

Mzee wa makamu anaendelea kuuguza majeraha ya mbavu baada ya kuanguka katika shimo linaloendelea la choo akifukuza kipungu aliyechomoa samaki mkubwa katika pakacha lake.

Kisa hicho cha kusikitisha kilifanyika katika kijiji kimoja sehemu hii majira ya asubuhi baada yam zee huyo kukseha mtoni akivua samaki.”Alikuwa ndio mwanzo anaanza kuwatayarisha samaki wake wakati kipungu huyo(Aina ya mwewe mkubwa) alifika na kunyakua samaki mkubwa katia ya wote.” Akasema kijana wa mzee huyo alipokwua akiongea na mdokezi huyo.

Kuona samaki mkubwa akienda na kipungu huyo hakukumfurahisha buda ambaye bila kufahamu yaliyomngoja alifululiza mwendo kumkimbiza kipungu huyop ambaye hata hivyo aliendelea kupaa juu mbio mbio.Ni katika kimbia kimbia hizo ndipo mzee alijipata akianguka ndani ya shimo na kuumia mbavu.Kilio cham zee akiomba usaidizi kiliwafikia majirani ambao walifika mbio na kumtoa huku akiendelea kuguna na kupiga kite.

”Haki ya mungu kipungu huyu nikimpata nitammaliza.” Akaendelea kulia mzee huyo kabla ya kukimbizwa katika zahanati ya karibu ambapo alitibiwa.Hata hivyo kulingana na kijana wake,mzee huyo sasa anaendelea na nafuu baada ya kubainika kuwa alipata mikwaruzo tu wala hakuvunjika mbavu.

Mwisho.

DONDOO

JIJINI MOMBASA.

Sekrtari ambaye alikuwa ameaminiwa mno na mdosi hadi kufikia hatua ya kukingiwa makosa yoyote na mkurugenzi huyo sasa amemwaga unga baada ya bosi kugundua kuwa msichana huyo wa afisini mwake amekuwa akimdokezea mama watoto na baadhi ya maadui wake wa biashara baadhi ya siri muhimu za kazi yake.

Kuligana na mmoja wa wanfanyikazi ambaye alikuwa wa kwanza kupata habari hizo kabla ya kumjulisha mwana dondoo wetu,ni kuwa msichana huyo baada ya kupata kazi ya kuwa sekretari wa bosi amekuwa akijivuna mno na kuwaona wafanyikazi wenzake kama vidudu mtu ambao kamwe hawawezi kumfikia pale alipo.Kwa maana hiyo,amekuwa akiringa huku hata akifanya makosa mdosi anakuwa mtu wa kwanza kumtetea dhidi ya tuhuma.

Hata hivyo juzi,mdosi alishtuka alipopata habari za siri ya kampuni yake katika afisi jirani ambayo wanafanya kazi sawia.Hapo ndipo alipouliza kwa makini na kwa ujasiri wa hali ya juu akafahamishwa kuwa ni sekrtari huyo ndiye ambaye amekuwa akitoa siri zake kwa mdosi jirani na kuchotewa kiasi kikubwa cha fedha.

”We bwana unasemaje,sisi tunanunua hizi habari zako kutoka kwa sekrtari wako.” Akasema meneja katika kampuni jirani.Ndipo akaanza uchunguzi na muda sio muda akampata demu huyo akitoa ripoti ya fedha kwa afisi jirani.Hapo bila kusita alimfuta kazi papo hapo na asa demu anahaha kwa kukosa kazi.

Mwisho.

DONDOO

LIKONI-MOMBASA.

Jamaa ambaye aliamua kuwachukua watoto wake sita hadi katika kituo cha kuwatunza mayatima kwa dai kuwa hana lolote maishani sasa amerudishiwa watoto wake baada ya wasimamizi wa kituo hicho kugundua kwamba buda huyo alitaka mwanya wa kuwa pekee ili aendelee kuponda maisha na vipusa mitaani.

Cha ajabu na ambacho bado kimewashanza wengi ni jinsi mzee huyo alivyoweza kuwateka akili wenye kituo hicho na kuonekana kuwa mtu aliyezongwa na mashaka tele huku akiwa katika hatua zake za mwisho duniani.

”Alifika kituoni kama mtu ambaye anakaribia kufa na alionekana kukata tama kabisa ndipo tukawachukua watoto hawa baada ya kutuelezea kuwa mkewe alifariki miaka miezi sita iliyopita.” Akasema mmoja wa walezi kituoni hapo.

Hata hivyo juhudi za wenye kituo kufumbua fumbo la buda huyo mjanja hazikuchukua muda mrefu kwani kalameni alibambwa katika klabu kimoja cha usiku akila raha na vimwana mtaani humu.

Vile vile pindi tu bibi alipoata habari hiyo aliamua kufika kituo cha mayatima na kukutana na wanawe ambao walikuwa na hamu ya kumuona mama yao.

Hapo ndipo wenye kituo walitaka kufahamu kama mzee alisema kweli kuwa mama alifariki lakini mama huyo akasitiza kuwa ni yeye ndiye mwenye watoto hao na kwamba yupo hai isipokuwa alikuwa ameachana na mzee huyo kutokana na tabia yake ya kupenda viwwana wadogo wadogo.

Hapo ndipo buda alinaswa na kurudishiwa watoto hao huku aiambiwa alipie gharama ya watoto hao au afungwe jela.Ingawa alitaka kujitetea buda aligundua kuwa mambo yalikuwa magumu na akakubali uamuzi wa jopo la kijiji.

Mwisho.

DONDOO

KIWEIRERA-LIKONI

Buda ambaye hupenda pombe kuliko masuala yoyote ya nyumbani juzi alikuwa kicheko cha asubuhi kwa wakazi wa sehemu hii baada ya kuuza kitenge cha WAX cha mama watoto ili kulipia deni la pombe aliyokunywa siku mbili zilizopita.

Ilidaiwa kuwa mzee huyo alikuwa amemhadaa muuzaji wa pombe hiyo kuwa angelipata fedha zake kwa muda wa siku mbili ila tu kufahamika kuwa hata jamaa kumbe ni kibarua tu na hana kazi ya kudumu.

Ahadi yake ilitokana na kibarua ambacho alikuwa akipata katika muda huo lakini akashtuka kuamibiwa kuwa laini ilikuwa imekatika.Ndipo asubuhi hiyo muuzaji pombe akabisha hodi na juhudi za polo kutaka kutorokea na mlango wa nyuma zikakwama baada ya mlango huo kuufungwa kwa kufuli na mwenye nyumba.

Kuona hataweza kukabiliana na mama muuzaji,jombi aliamua kutoa lile rinda la kitenge,ambalo ni mojwapo ya marinda ambayo mama watoto huyapenda sana akienda katika mikutano ya akina mama kijijini.

Yote haya yakifanyika mama watoto alikuwazake sokoni Kongowea na aliporudi mwendo wa saa nne,akagundua mara moja rinda lake la kitenge.Hapo aliuliza na huku mzee akisita kuongea,majirani walisema kuwa bwana huyo alitoa rinda hilo kwa muuzaji pombe ya kienyeji.Lo hasira kweli ni hasara kwani mama watoto alishindwa kujizuia na kuanza kumimina mvua ya makonde kwa polo huyo hadi akazimia.Pia hakuachia hapo alifululiza hadi kwa muuzaji pombe ambaye alitorokea dirishani alipomuona bibi ya polo akienda.Haikufika jioni,mama alikuwa amepata kitenge chake huku mzee akiwa na majeraha.

Mwisho.

DONDOO

MIKANJUNI-JOMVU.

Kalameni mmoja katika eneo hili ambaye wakati Fulani alijipata katika hali ya kutatanika baada ya kukojolewa na paka akiwa amelala na mkewe sasa anadai huo ulikuwa ni urogi wa wazi baada ya kushindwa kabisa sasa kujamiana na mkewe.

Akiongea na mdokezi wetu,kijana huyo wa makamu ambaye kwa sasa ana watoto wawili alisema kuwa masaibu yake ya kufanya tendo la ndoa yalianza siku chache tu baada ya kukojolewa na paka huyo akiwa amelala na mkewe.

“Mimi sasa sina raha kabisa,ninajaribu kujua kilkichofanyika na kila mganga ambaye ninapata fursa ya kwenda kwake anasema jogoo langu lilipata mshtuko kutokana na urogi huo na sasa huenda sitazalisha tena maishani.” Akasema kwa huzuni.Aidha alisema kuwa amekuwa akifika kwa madaktari mbalimbali lakini anaamibiwa kuwa mambo yatakuwa shwari ila tu hakuna kinachofanyika.

Huku akionekana kama mwenye mfadhaiko wa mawazo kuhusu shida hii,kijana huyo alisema kuwa anaamini hili lilikuwa tukio la urogi ingawa hajafahamu kamwe kama ni nani ambaye ni mhusika mkuu katika tatizo hili.

”Sitasema kumaliza roho yangu lakini ukweli wa mambo ni kuwa mimi nilirogwa kwa sababu nilikuwa nikitimiza majukumu yangu vizuri nikiwa kitandani lakini sasa yanayotokea yananitia wasiwasi.” Akasema.

Mwisho.

DONDOO

KIWANDANI-KILIFI.

Jamaa ambaye anajulikana sana mtaani kwa wivu usiomithilika sasa ameamua kuacha kazi na kubaki na mkewe nyumbani kwa vile amekuwa akidai kuwa mkewe hugawa tunda lake pindi tu anapoondoka kwenda kazini.

”Sitataka tena kwenda kazini kwa vile kila nikienda kazini mke wangu naye hufuatwa na vijana barobaro na hilo ni jambo ambalo katu siwezi nikalikubali katika maisha yangu.” Akasema baada ya kuhojiwa shida ya yeye kuacha kazi.

Majirani ambao waliongea kuhusu tukio hilo walisema kuwa kijana huyo amekuwa na shida zinazohusiana na masuala ya kinyumbani na mkewe na zaidi sana ikiwa ni wivu ambao umeshindwa kumuondokea polo huyo.

Vile vile juhudi za kijana huyo kufika katika kongamano za kijamii ili kuelezewa kuhusu uhalisia wa maisha pia zimekuwa bure bilashi kwani huwa kila aambiwalo haamini na hivi kwamba amejenga taaswiri hiyo kumhusu mkewe.Ndipo sasa inadaiwa kuwa bibi naye ameamua kuwa sasa ni afadhali aondoke na sasa jamaa amebaki kapera huku fauka ya haya akiwa pia hana kazi.

Mwisho.

DONDOO

MOI AVENUE-MOMBASA.

Kulikuwa na kituko cha muda kilichosimamisha shughuli za kibiashara katika barabara hii baada ya jamaa mmoja aliyekuwa na hasira za mkizi kuamua kutokubali demu aliyekuwa akiburudika naye kumuondokea baada ya kupata mwenye hela zaidi.

Kisanga hiki kiliwapata wakazi wa jiji la Mombasa ambao walikuwa wakiregea majumbani mwao baada ya shughuli za siku wakiwa na mshangao mkubwa huku demu na polo wakifukuzana kama watoto wadogo.

”Kwanini sweetie unaenda ni mimi niliyeanza nawe sasa mbona unaniacha kwa huyo jamaa.” Akalia polo huku demu akiwa ameshikana mkono na jamaa aliyeonekana kuwa amejaa hela hasa kutokana na jinsi alivyokuwa amevaa.Kwanza polo alikuwa amevaa bling za bei mbaya na alidhaniwa kutoka jijini Nairobi.

Awlai ndani ya mkahawa kulimoanza vituko,wahudumua walisema kuwa demu aliingia akiwa na kijana wake ambye hata wao wamezoea lakini ghalfa akaingia jamaa huyo aliyekuwa amejikwatua kwa viwalo vya pesa mbaya na kufululiza hadi pale alipokwua msichana.

Baada ya maongezi machache waliondoka wote na kumuacha kijana wa Mombasa akiwa hajui atafanya nini.Hapo ndipo kijana akaanza kulia na kumfuata jamaa mbio hadi nje ambako nako ilikuwa kasheshe tele hadi walipopotela katika eneo la Mwembe Tayari.Haikujulikana hatima ya polo huyo ila wengi walidhani huenda demu huyo hakuwa na mapenzi ya dhati kwa kijana huyo wa Mombasa.

Mwisho.

Comments