Mkulima stadi sana wa kilimo cha mboga katika sehemu ya Vikwathani-Mombasa.







Mzee Samson Kitony akishuhgulikia shamba lake katika eneo la Vikwathani huko viungani mwa mji wa Mombasa.huyu ni mkulima stadi mno katika kilimo cha kisasa.


SAWASHANGAZA WAKAZI KWA KILIMO CHA KISASA VIKWATHANI


Safari nyangu kuelekea katika kijiji cha Kadzondzo viungani mwa kituo cha biashara cha Mishomoroni,katika eneo bunge la Kisauni ilikuwa na lengo moja tu;kuonana na mkulima ambaye mbinu zake za kisasa za upanzi wa mboga zimekuwa jambo la kushabikiwa kijijini hapa.

Hata hivyo safari yangu kueleka huko haikuwa rahisi na ilihitaji ari ya kutaka kufika huko.Kwanza muindo duni ya barabara iliyochakaa kwa matope ndilo jambo ambalo nilikumbana nalo.Kuna utelezi mwingi na hali ilionekana kunitatiza sana hasa kwa vile kulikuwa kumenyesha alasiri hiyo.Mbali na haya yote,kuna vilima na vijito ambavyo vinahitaji tahadhari kuvipitia.

Na safari yangu ya saa moja unusu ikafikia katika shamba kubwa la Mzee Solomon Simba Kitony,mhandisi mstaafu katika idara ya ujenzi wa barabara huko Kangundo.Na nilipofika kwake,nilikutana na mzee huyo akiwa ndano ya bohari lake ambalo amepanda nyanya ambazo tayari zimeanza kuwa tayari kwa kuvuna.

Awali sikufahamu kule aliko hadi mfanyikazi wake aliponieleza kuwa mzee huyo alikuwa ndani ya bohari hilo la nyanya akikagua mimea hiyo.Nami nikabisha hodi ili kuonana na mzee huyu ambaye majirani wanasema ameleta ina mpya ya ukulima ambao haujawahi kuonekana katika sehemu hii ya Vikwathani na eneo kubwa la pwani kwa ujumla.

Mzee Kitony ameamua kutumia aina ya ukulima ambao unajulikana kwa kimombo kama Greenhouse Farming.Huu ni ukulima ambao unatumika sana katika maeneo ya Naivasha katika ukuzaji wa maua lakini mzee huyu kama alivyoongoea na Taifa Leo,yeye anaamini kuwa hata mimea mingine inaweza kunawiri vyema ikikuzwa ndani ya bohari.

“Wengi walishangaa nilipojenga bohari hii na kuanza kupanda nyanya lakini sasa wamegundia kuwa mbinu hizi pia husaidia mimea mingie wala sio tu maua kama inavyofanyika katika mashamba makubwa yaliyoko Naivasha.

Hivyo kutokana na kilimo hiki,mzee Kitony sasa anatarajia kupata mavuno mema katika msimu huu hasa baada ya nyanya zake kunawiri vyema ndani ya bohari hili.”Kwa kweli sasa ninatarajia kupata mavuno mazuri ingawa hii ndiyo mara yake ya kwanza kulima kwa kutumia ukulima huu.

Hata hivyo lililonishangaza nikuwa mzee Kitony kamwe hajawahiku kuhusika na mausala ya kilimo na kwamba muda wote wa awali aliutumia akiwa katika shuhguli zake za uhandisi katika idara ya ujenzi huko Kangundo.”Mimi kwa kweli awali nilikuwa kijihusisha na masuala ya barabara lakini kadri muda ulivyozidi kuyoyoma,ndipo nikapata ari ya kutaka kufanya kazi za ukulima.” Akamweleza mwandishi wa makala haya katika shamba lake.

Mzee Kitony alifanya kazi na serikali kuanzia mwaka wa 1980 akiwa mhandisi wa barabara hadi alipojiuzulu kazi hiyo mwaka wa 1990 na papo hapo akaanza kuingilia masuala ya ukulima.”Niliamua kuacha kazi ya kuajiriwa ili niendeleze ndoto yangu ya kuwa mkulima na hali hiyo ikajitokeza mwaka wa 1990 nilipoamua kustaafu na kuamua kuingilia kilimo.” Akasema.Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuanza shughuli za ukulima katika sehemu ya Kangundo katika wilaya ya Machakos.Mwaka wa 1991 alianza kwa kupanda mboga lakini pia akaamua kukuza maua katika shamba lake mwaka wa 1993.Na ili kukidhi aru yake katikas shughuli hizi,Mzee Kitony alianzisha ufugaji wa kuku mwaka wa 1994,shughuli ambayo iliendelea kumpa pato lake la maisha kabla ya kuingilia ufugaji wa ngombe na kutimiza kabisa ari ya Kitony kuwa mkulima wa kutajika katika sehemu ya Kangundo.

Na ili kukidhi hamu ya wateja wake ambao walikuwa wakifurika kwake wakitaka kuuziwa maziwa,Mzee Kitony aliamua kuanzisha duka la kuuza maziwa katika kituo cha biashara cha Tala katika eneo hilo la Kangundo.”Watu walikuwa wamejua kuwa ukifika kwangu utapata maziwa na nilikuwa na idadi kubwa ya wateja na hapo ndipo nikaamua kufungua duka katika kituo cha biashara cha Tala katika eneo la Kangundo ili kuwahudumia wakazi wa huko,na kweli biashara ilizidi kunawiri..” akasema kwenye mahojiano na Taifa Leo.

Hata hivyo baada ya miaka mingi ya kuishi na kutoa huduma zake katika sehemu ya Tala,huko Kangundo,mzee Kitony aliamua sasa ateremke pwani na kuendeleza kilimo hiki.Na safari yake ya mwaka jana ikamfikisha katika sehemu hii ya Kadzondzo ambayo inapakana kwa karibu na mtaa maarufu wa Vikwathani.

Sio wengi waliogundua kuwa mzee huyu ni mkulima wa kisasa hadi alipoamua kustwasha eneo la shamba alilopta karibu na kilima katika sehemu hii.”Nilipofika hapa mwaka jana niligundua kuwa eneo hili lina rotuba tele lakini wenyeji wanaamua kukuza tu mahindi pekee badala ya kuzingatia kilimo cha mboga na matunda,na hapo ndipo nikaamua kuanza kukuza mboga hizi.” Akasema akimuonyesha mwandishi huyu sehemu kubwa ambayo amepanda sukuma,biringanya na takribani kila aina ya mboga.

Na ili kufanikisha zoezi zima la kukuza kilimo hiki,Mzee Kitony aliamua pia kuchimba kisima ambapo yeye huchota maji na kunyunyizia shamba lake.Na ndani ya bohari maalum ambalo anakuzia nyanya zake,ameweka mifrereji ambayo hupiga maji moja kwa moja kutoka ndani ya kisima.

Pia Mzee Kitony ameajiri vijana wawili ambao wanamfanyia kazi ili kuhakikisha kuwa kilimo chake hiki kinanawiri vyema na kumletea faida.anataraji hivi karibuni kuvuna nyanya zake na kuzipeleka sokoni ambao atapata bei nzuri.Alisema kuwa kwa ssa nyanyna ni mojawapo ya mboga ambazo zinaleta faidi nzuri mno.

Alisema mpango huu wa kupanda na kukuza mboga ndani ya bohari unasaidia mimea kukwepa wadudu waharibifu ambao hupatikana hewani bila kuonekana.

Aliongeza kuwa katika mkoa huu wa pwani,magonjwa ya hewa ambayo huumiza mimea imezagaa hasa kulingana na hali ya anga ambayo ni ya joto na hivyo akasema ipo haja kwa wakazi wa sehemu hizi kujaribu mbinu kama hizi za kilimo ambazo mwishowe zitawafaidi.”Kwa sasa ni wazi majaribio yangu ya kutumia aina hii ya kilimo ina afyeni kwani tayari nyanyna zimeiva vizuri na hivi karibuni nitazipeleka sokoni ili ziuzwe nipate riziki.” Akasema.

Na baadhi ya wakazi wa Kadzondzo ambao Taifa Leo iliongea nao walifurahia juhudi za Mzee Kitony ambaye sasa ukulima wake na mbinu hizi ni gumzo kila mtaa unaoenda.”Kweli tunaona huyu mwenztu amejiri na mbinu bora za kilimo ambacho kikifuatuliwa vyema basi kinaweza kutufaidi hasa katika eneo hili ambalo limejaa rotuba.” Akasema Mzee Peter ambaye ameishi katika sehemu hii kwa muda mrefu.

Hadi nikiondoka katika shamba la mzee Kitony,nilikuwa nikijivunia juhud ihizi kubwa za mkulima huyu ambaye anasema haoni chochote cha kumsimamisha hadi ndoto yake ya kuwa mkulima mtajika itimie.

Mwisho.

Comments