NJAA INAVYOWASUMBUA WAKAZI HUKO KILIFI MKOANI PWANI.





























Hivi majuzi nilizuru maeneo ya mashambani mwa wilaya ya Kilifi katika mkoa wa pwani na kile nilichokumbana nacho kilikuwa dhahiri.Hali hali ya maisha ya wakazi wengi huku inatia hofu kutokana na baa la njaa.














Ingawa serikali inajaribu kuwasaidia kwa kutuma chakula cha msaada,hali haijakuwa na afyeni hivi kwamba wakazi wengi bado wanakodolea macho kifo kutokana na baa hili la njaa.














Kulingana na mahojiano niliyofanya,wengi hawajavuna chochote katika mashamba yao kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.Na sasa wanataka serikali iwasaidie hata zaidi.














Mwaka wa 2005,taasisi ya kukadiria hali ya umaskini nchini ilizindua ripoti yake ambayo ilionyesha kuwa eneo la Ganze ndilo lenye kiwango kikubwa cha ukata na umaskini uliokithiri.














Tafadhali saidieni wakazi hawa nao wawe na angaa tone la furaha maishani mwao.Picha zinaonyesha hali ilivyokuwa wakati wa kugawanywa kwa chakula hicho cha msaada katika shule ya msingi ya Mnagoni wilayani Bamba.














Kazungu.

Comments

Unknown said…
Pongezi kwa kazi yako nzuri kaka umejikakamua vilivyo kutupasulia mbarika ya njaa ya kilifi; lakini mbona umekua ja mwamba ngoma wavutia kwako pekee.Pia ungezungumzia sehemu za Kinango,Kwale na hata eneo bunge la Msambweni.
Kazungu Samuel said…
Niko na ripoti za Kinango pia. Nimewahi kuwa huko. Naelewa hali halisi kwa hivyo nitachapisha pia.
Ahsante kwa kuingia na kujionea matatizo ya watu maeneo ya mashambani