GOVERNOR JOHO ASEMA ATAWANIA URAIS KENYA MWAKA WA 2022

Gavana wa Mombasa Bw Hassan Joho amesema kuwa atawania Urais wa Kenya mwaka wa 2022.
Akiongea siku ya Jumapili katika eneo la Mtomondoni, Mtwapa wakati wa harambee kusaidia watoto wasiojiweza kupata elimu, Gavana huyo alisema kuwa mara hii, lazima mwaniaji wa Urais atatoka katika eneo la Pwani.
"Kile ninachojua ni kuwa ikifika wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2022, eneo la Pwani pia litatoa mwaniaji wa Urais. Kama tutaanguka, lakini mara hii ni lazima tuanguke tukiwa katika debe la Urais," akasema Bw Joho.
Gavana huyo ambaye pia ni naibu wa kiongozi wa chama cha ODM amekuwa akizunguka katika maeneo mbalimbali ya taifa la Kenya akitaka uungwaji mkono.
Kama kiongozi ambaye yuko karibu zaidi na kinara wa chama hicho Bw Raila Odinga, gavana Joho yuko na matumaini mengi ya kufaulu kupata uungwaji mkono kutoka kwa Bw Raila.










Picha ya hapo juu ikimuonyesha gavana wa Mombasa Bw Hassan Joho(wa pili kutoka kulia) akiwa na baadhi ya viongozi katika harambee ya kusaidia wanafunzi werevu kutoka jamii maskini katika shule ya msingi ya Mtomondoni siku ya Jumapili.Picha na Kazungu Samuel

Comments