WAKAZI WA SHIMONI, KWALE WASEMA UKUTA UTAKWAMISHA BIASHARA ZAO


Baadhi ya wakazi wa eneo la Shimoni, kaunti ya Kwale sasa wameeleza hofu yao kwamba ukuta ambao unajengwa na serikali ya kitaifa utawazuia kufika baharini.
Wengi wa wakazi hao ambao ni wavuvi walisema kuwa endapo hakutakuwa na mawasiliano kutoka kwa serikali, jambo hili litawatatiza.
Wakazi hao waliongea kupitia kwa mwenyekiti wa kikunbdi cha maendeleo cha Shimoni Bw Mohamed Shee.
“Sisi tulisikia kwamba kutajengwa ukuta lakini serikali haijakuwa na uwazi na sisi. Sasa tunajiuliza ni jambo gani ambalo linaendelea sasa. Ombi letu ni kuwa tutasikilizwa kama wakazi wa Shimoni,” akasema Bw Shee.
Hata hivyo akiongea na mwana blogu huyu, msaidizi wa kamishna wa kaunti ndogo ya Lunga Lunga Bw Josphat Biwot alisema kuwa atafanya mkutano na wakazi ili kujadiliana kuhusu hatima ya suala hilo.
“Tutakuwa na mkutano na wakazi ili tujue hasa ni jambo gani ambalo tunafaa kuliendeleza. Tuko na kibarua cha kuhakikisha kwamba kila mkaazi anasikilizwa,” akasema Bw Biwot.














Hili ni egesho katika bandari ya Mombasa. Katika eneo la Shimoni, kaunti ya Kwale kunatarajiwa kuwekwa ukuta ili kuzua visa vya biashara ya magendo. Picha na Kazungu Samuel

Comments